Kote ulimwenguni ,viwanda vya kaa jiwe ,pamoja na ulafi wa viwanda vya visukuku  vinatishia maeneo ya kitamaduni na ya kiasili yasioweza badilishwa.

Ndani ya Lamu,serikali ya Kenya pamoja na Kampuni ya Amu Power,wanajenga kiwanda  cha megawati 1,050 cha kaa jiwe,ndani ya kaunti ya Lamu,kilicho kisiwa kando ya pwani ya Africa Mashariki,Kaskazini mwa Mombasa,nchini Kenya.Eneo la Urithi wa dunia la UNESCO na nyumbani kwa eneo kale la makaazi ya Wasawahili  yaliyohifadhiwa kuhifadhiwa.

Ule mradi wa dola billion 2 uliopendekezwa utaongezea kiwango cha uzalishaji wa gesi chafu ,kwa asilimia 12/12%,wakati nchi ilitoa nia ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu  hadi asilimia 30/30%,kufikia mwaka wa 2030.

Tusikubali eneo hili la thamani libadilishwe na kaa jiwe uchafu.Athari za kimazingira kutoka kwa kiwanda cha kwanza cha Kenya  cha stima ,kinachoendeshwa na kaa jiwe ,kitaharibu milele mazingira tete ya kisiwa hicho ,na kutishia riziki ya karibu watu 120,000 wanaoishi katika kaunti ya Lamu.

Onyesha msaada wako kwa watu  wa Lamu. Jisajili katika ukurasa wa kuomba,waambie UNESCO  unavyohisi/maoni yako juu ya mradi mpya wa kaa jiwe ,ulio katika eneo la urithi uliohifadhiwa,ambao utaongeza mabadiliko ya tabia nchi,na kuharibu urithi wa kizazi cha baadaye.

FacebookTwitter